Asante Magufuli kwa kazi nzuri!!!!
Kazi nzuri Makonda.
Kwa mijibu wa RC Paul C. Makonda, Wilson
Kabwe alisainisha mikataba miwili kwa wamiliki
wa mabasi kwa sheria mbili tofauti (ya mwaka
2004 na 2006). ByLaw ya 2004 inataka bus
likitoka Ubungo lilipe Sh.4,000/= na ya 2006
inataka bus lilipe Sh.800/=.
Wamiliki wa mabasi walisainishwa kulipa 8000/=
lakini jiji likarekodi kuwa wanalipa Sh.4000/=.
Maana yake ni kuwa kila bus lilikua likilipa
Sh.8,000/=, lakini zilizokua zikiingia Halmashauri
ya jiji ni Sh.4000/= tu. Nyingine ziliingia mfukoni
kwa Kabwe.
Kwahiyo katika magari 400 yanayotoka Ubungo
kwa siku Kabwe alikua anaingiza 1,600,000/= kila
siku mfukoni mwake. Hizi ni sawa na Milioni 48
kwa mwezi. Sawa na milioni 576 kwa mwaka.
Hii ni moja ya tuhuma kadhaa alizozieleza
Makonda. Kwa kifupi Kabwe ni mpiga dili. Hata
kule Mwanza alipiga dili nyingi akawa analindwa
na "mkwere".. Kupitia dili hizo alijenga vitega
uchumi kadhaa ikiwemo "Royal Sunset Beach"
kule Luchelele.
Hebu jiulize kama kwenye dili moja tu ya mabasi
Ubungo anatengeneza Milioni 576 kwa mwaka,
ukijumlisha na hizo dili nyingine ana earn kiasi
gani? Ni ajabu kama tutamtetea mtu mwenye
tuhuma kama hizi.
Yani wakati wewe una mwaka wa 4 unatafuta
kazi bila mafanikio hata nauli ya kutembeza CV
yako huna, mwenzio anaingiza Milioni 500+ kwa
mwaka kupitia dili moja tu. Hakika utakua
"zwazwa wa shahada ya juu ya uzamivu (PhD)"
kama utamtetea.
Najua kuna "principle of natural justice" lakini hizi
natural justice ndio zimetuharibia nchi na
kutufikisha hapa tulipo. Mtu anaiba hela halafu
anaundiwa Tume imchunguze na tume inalipwa
tena hela. No. Si sawa.!
Naunga mkono Maamuzi ya Rais Magufuli
kumuweka kando huyu Mkurugenzi mwenye
tuhuma lukuki. Tangu akiwa jiji la Mbeya,
Mwanza na hatimaye Dar amekuwa akituhumiwa
tu.
Ezekia Wenje amewahi kumlalamikia bungeni,
Kiwia amewahi kumlalamikia bungeni, viongozi na
wananchi kibao wamewahi kumlalamikia lakini
hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake.
Leo kaambiwa akae pembeni kupisha uchunguzi
mnamtetea? Mtakuwa mmelogwa walahi.!
Kwanini atuhumiwe yeye tu? Haiwezekani watu
wote wamchukie yeye tu.
Makonda kafanya jambo la msingi sana leo kuliko
wakati mwingine wowote ktk historia yake.
Katetea machozi ya wanyonge. Kakatisha dili za
watawala kujishibisha kwa kutumia migongo ya
maskini.
Kampeleka Kabwe kwa Pilato, na Pilato
akawauliza watu nimfanyeje mtu huyu.. wakapiga
kelele wakisema "asulubishweeee".. Pilato
akamsulubisha. Sasa mnataka natural justice
kwny tuhuma zilizo wazi?
Apumzike pembeni uchunguzi ufanyike kama
alivyosema Rais. Na iwe fundisho kwa wezi kama hao.
Comments