Posts

Showing posts from August 30, 2015

Je!!!!!! unapenda kufahamu SANDUKU LA AGANO LIKO WAPI?????????

Image
SANDUKU LA AGANO LIKO WAPI? Huu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt ( Misri ) wakielekea promised land ( Nchi ya ahadi ). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa ( acacia wood ) iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7 metres na kimo cha 0.7 metres. Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi. Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo (" hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni patakatifu pa patakatif...