Posts

Showing posts from May 31, 2016

WAFAHAMU WACHAGA NA TAMADUNI ZAO

Image
Kabila la Wachaga linafahamika kwa wengi kuwa linapatikana mkoani Kilimanjaro. Kwa asili, Wachaga ni mchanganyiko wa Wamasai, Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe. Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya 17. Walipofika wakiwa katika vikundi vidogovidogo waliwakuta wakazi, wenyeji kwenye Misitu ya Mlima Kilimanjaro walioitwa Wakonyingo. Wenyeji hawa ambao huitwa Mbilikimo hawakupenda kuchanganyika na wahamiaji wageni, hivyo wakahama na kuanzisha makao yao ya kudumu kwenye misitu minene iliyopo nchini Kongo. Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga 2,000,000. Vikundi vya Wachagga Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano ya...